SACP. AHMED
Z. MSANGI
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya
|
Wanachuo wawili wa mwaka wa kwanza Dipoma ya Business Administration wa chuo cha mzumbe kampasi ya mbeya, wakazi wa forest
ya zamani hosteli za nje waliotambuliwa kwa majina ya Michael tarimo (20) na Albert
shenkalwa (23) walikufa maji
baada ya mtumbwi waliokuwa wanautumia kupigwa maji, kupinduka na wao kushindwa
kuogelea.
Tukio
hilo limetokea mnamo tarehe 02/05/2014
majira ya saa 9 alasiri huko katika
zoo ya wanyama iliyopo katika hospitali teule ya ifisi – kata ya songwe, tarafa
ya bonde la usongwe, wilaya ya mbeya vijijijini. wanafunzi hao wakiwa na wenzao 12 walikwenda eneo hilo kwa ajili ya picknic na kuangalia wanyama na baadae kwenda
kwenye bwawa linalotunza samaki na kuanza
kuingia ndani ya bwawa hilo kwa kutumia mtumbwi huo kwa zamu.
katika bwawa hilo watu hawaruhusiwa kuogelea isipokuwa kuingia kwa mtumbwi.
Kamanda
wa polisi mkoa wa mbeya kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed z. msangi anatoa wito kwa jamii
kuwa makini na mazingira wanayokwenda kutembmelea ili kuepusha madhara
yanayoweza kuepukika.
No comments:
Post a Comment