Wakazi
wa wilaya ya Tunduru wakigawana nyama ya Kiboko huku mmoja akimnyooshea
mwenzie fimbo baada ya jamaa kutaka kuleta fujo wakati wa kugawana
nyama hiyo.
Nyama ya kiboko huyo ikiwa katika ndoo tofauti tofauti na nyingine ikiwa imewekwa chini.
WANANCHI wa Mji wa Tunduru Mkoani Ruvuma wamemuua Kiboko aliye muua Mkazi wa Kitongoji cha Chacha katika Kijiji cha Mhuwesi katika kata ya Mhuwesi Tarafa ya Nakapanya Marehemu Njaidi Selemani Njaidi (70) na kumla nyama yake bila kujali dini zao.
Katika kuonesha kuwa Mnyama huyo analiwa na waumini wa dini zote Maelfu
ya wananchi walijitokeza kumlinda asitoke hadi usiku wa saa 9
walipotokea askali wa idara ya wanyamapori na kumpiga risasi. Aidha hali
ilikuwa tete baada ya Kiboko huyo kuuawa ambapo mamia ya vijana
wenyeguvu walijitokeza na kujitosa katika bwawa hili na kuanza
kumshambulia kwa kutakata nyama hiyo huku wakiwa wanagawana na mwisho
kikaja Kivutio amakioja cha kuwatishia visu askari wa idara hiyo na
kuwapora ndoo 8 za nyama hiyo ambayo iliandaliwa kwa ajili ya kuondoka
nayo .
Kiboko huyo ambaye alimuua Marehemu Njaidi April 20 mwaka huu wakati akijaribu kukata kitoweo cha nyama baada ya kumkuta akiwa amelala katika eneo la shamba lake katika eneo la Mto Muhuwesi aliuawa na Askali wa Idara ya Wanyama pori katika eneo la Mto Nanjoka mjini Tunduru baada ya Wananchi hao kumzuwia asitoke katika bwawa lililopo kandokando ya mto huo kwa zaidi ya masaa 20.
No comments:
Post a Comment