Pichani
kuanzia kushoto ni Mama mzazi wa Mboni Masimba halafu Mboni mwenyewe
pamoja na mtoto wa marehemu anaitwa Sonia akiwa na mama yake Monalisa.
Sehemu
ya Wacheza Filamu nchini waliokuwa wamebeba Jeneza lenye Mwili wa
Marehemu George Otieno Okomu (George Tyson) wakijipanga tayari kwa akili
ya kuongoza shughuli ya Kuga mwili iliyofanyika kwenye viwanja vya
Leaders Club,Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.Mwili huo umesafirishwa
kupelekwa nchini Kenya ambako ni nyumbani kwao na Marehemu kwa ajili ya
mazishi yatakayofanyika Jumamosi ijayo baada ya kukamiliza kwa mipango
yote.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Saddick akiwaongoza waombolezaji
mbali mbali kwenye shughuli ya kuaga mwili wa Marehemu George Otieno
Okomu (George Tyson) waliofika kwa wingi kwenye viwanja vya Leaders
Club,Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Kipindi cha The Mboni Show,Mboni Massimba (kulia) akiwa ni
mwenye huzuni sana kwa kuondokewa na Mwaznilishi mwenza kwa Kipindi
chake hicho ambaye alifariki Dunia katika ajali ya Gari huko Mkoani
Morogoro wakati wakitokea Mkoani Dodoma kukabidhi msaada wa Madawati
katika moja ya shule za msingi zilizopo mkoani humo ikiwa ni maadhimisho
ya Miaka miwili ya kipindi hicho.
Aliekuwa
Mke wa Marehemu George Otieno Okomu (George Tyson),Yvone Chelly
(Monalisa) na Mwanae Sonia wakiwa ni mwenye Majonzi makubwa kwa
kuondokewa na mpendwa wao.Kushoto ni Mama wa Monalisa,Bi. Natasha.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Saddick akitoa nasaha zake wakati wa msiba huo.
No comments:
Post a Comment