Pages

Saturday, July 5, 2014

NEYMAR AUMIA UWANJANI,KUIKOSA NUSU FAINALI DHIDI YA UJERUMANI


Neymar akiwa amelala chini baada ya kupata majeruhi 
NYOTA wa Brazil, Neymar,  ataikosa mechi ya nusu fainali baina ya wenyeji dhidi ya Ujerumani jumanne ijayo, hii ni kwa mujibu wa kocha, Luiz Felipe Scolari.
Taifa mwenyeji limefanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali baada ya ushindi wa mabao 2-1 mjini Fortaleza, lakini nyota wake alitolewa nje kwa machela dakika tatu kabla ya mechi kumalizika na amekimbizwa hospitali baada ya mechi kumalizika kutokana na kupata majeruhi ya mgongo.
Neymar amekuwa akijikaza kuimarika katika mechi zote za Brazil kutokana na majeruhi ya  goti, lakini alifaulu kuanza katika mechi zote.


No comments:

Post a Comment