Mwanamuziki TI wa Marekani akiingia kwenye ukumbi wa mkutano leo jioni hii kwenye hoteli ya Seacleaf wakati yeye pamoja na Mwanamuziki Davido wa Nigeria na wanamuziki wengine mbalimbali watakaoshiriki katika Tamasha la Serengeti Fiesta ni Sheeedah walipoongea na waandishi wa habari kueleze jinsi watakavyofanya mambo mamkubwa kwenye tamasha hilo linalofanyika kwenye viwanja wa Leaders Kinondoni jijini Dar es salaam.
Mwanamuziki TI wa Marekani akisalimiana na Mwanamuziki Davido wa Nigeria wakati walipokutana kwenye ukumbi wa mkutano tayari kwa kuongea na waandishi wa habari kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Bw. Steve Gannon.
Mwanamuziki TI wa Marekani kulia akisikiliza kwa makini wakati mwanamuziki Davido alipokuwa akizungumzia tamasha la Serengeti Fiesta ambapo pia ataimba nyimbo zake.
Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Bw. Steve Gannon akizungumzia mafanikio ya Tamasha la Serengeti Fiesta wakati wa mkutano na waandishi wa habari kushoto ni Mwanamuziki TI kutoka nchini Marekani na kulia ni Ephraim Mafuru Mkurugenzi wa Masoko SBL
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Tamasha la Serengeti Fiesta Bw. Sebastian Maganga akifafanua jambo katika mkutano huo leo
Ephraim Mafuru Mkurugenzi wa Masoko SBL akizungumzia burudani hizo katikati ni Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Bw. Steve Gannon kushoto ni Mwanamuziki TI kutoka nchini Marekani..
Kutoka kulia ni Ephraim Mafuru Mkurugenzi wa Masoko SBL, Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Bw. Steve Gannon, Mwanamuziki TI kutoka Marekani na Mwanamuziki Davido kutoka nchini Nigeria
Mkurugenzi wa Kampuni ya Clouds Media Bw. Joseph Kusaga akiwashukuru wanamuziki wote watakaoshiriki katika kutoa burudani, Kampuni ya bia ya Serengeti na vyombo vya habari kwa ushirikiano wao.
Mwanamuziki Victoria Kimani kutoka Nairobi nchini Kenya akizungumza katika mkutano huo
Mwanamuziki Davido akitia neno katika mkutano huo huku mwanamuziki TI akisikiliza kulia anayefurahia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti SBL.
Mtu mzima TI akimwaga maneno yake kwa wanahabari
Chanzo: Matukio na vijana.
No comments:
Post a Comment