Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipanga makabrasha tayari kuendesha kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ambapo masuala ya kujiendesha kiuchumi na mipango ya maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa yanajadiliwa.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa NEC mjini Dodoma ambapo aliwaeleza juu ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana Oktoba 16, 2014 katika siku ya kwanza ya kikao chake cha siku mbili kinachoendelea mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete imejadili na kupitisha Sera ya CCM ya kujitegemea kimapato na kiuchumi.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Halmashauri Kuu
ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana Oktoba 16, 2014 katika siku ya
kwanza ya kikao chake cha siku mbili kinachoendelea mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya
Mrisho Kikwete imejadili na kupitisha Sera ya CCM ya kujitegemea kimapato na
kiuchumi.
Sera hiyo
inalenga kuwa muongozo wa kuifanya CCM ianze kuzitumia rasilimali zake
kuzalisha ili iweze kujitegemea kiuchumi.
Aidha
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imefanya uteuzi wa wagombea kwa nafasi za
Uenyekiti wa CCM katika wilaya mbili pamoja na wagombea Ujumbe wa NEC katika
wilaya tatu zilizokuwa na nafasi wazi.
WALIOTEULIWA
KUGOMBEA UENYEKITI WA WILAYA NI;-
Wilaya ya
Njombe:-
Ndugu Edward Pius Mgaya
Ndugu Vallence Mtenzi Kabelege
Ndugu Betram Simon Ng’imbudzi
Wilaya ya
Misenyi:-
Ndugu Sosthenes Rweyemamu Kabandwa
Ndugu Said Ibrahim Seruh
Ndugu Erica Kiiza Stephen
WALIOTEULIWA
KUGOMBEA UJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA NI:-
Wilaya ya
Tandahimba:-
Ndugu Lutavi Abdula Suleman
Ndugu Malela Mohamed Chibwana
Ndugu Nanyundu
Ally Salum
Wilaya ya
Mkuranga:-
Ndugu Ally Mohamed Msikamo
Ndugu Maulid Hamis Zowange
Ndugu Wakati Nassoro Mtulia
Ndugu Zawadi Ally Kilapo
Wilaya ya
Njombe:-
Ndugu Christian Marcus Fwalo
Ndugu George Benedict Mng’ong’o
Ndugu Oscar Michael Msigwa
Ndugu Justin Nusulupia
Imetolewa na:-
Nape Moses
Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI
17/10/2014
17/10/2014
No comments:
Post a Comment