Pages

Friday, October 17, 2014

NAFASI ZA KAZI KUTOKA KWA WAKALA WA JIOLOJIA NCHINI TANZANIA(GST)

Taasisi ya Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) iliyo chini ya Wizara ya Nishati na Madini(MEM) imetoa nafasi arobaini na nne (44) za ajira kwa watanzania kupitia Ofisi ya Rais sekreterieti ya ajira utumishi wa umma.

Kwa mujibu wa Meneja Rasilimali watu na Maendeleo wa GST, Bw.Gabriel Kasase alimjulisha Afisa habari wa GST kuwa ajira hizo 44 zimegawanyika katika kwa kila idara ya taasisi ambazo alizitaja kuwa Idara ya utawala nafasi kumi na sita (16) , Idara ya Jiolojia nafasi kumi na moja(11) , idara ya Maabara nafasi nne (04) , idara ya KanziData nafasi nne (04) na kwa upande wa vyeo ni nafasi ya mkurugenzi nafasi tatu(03) , na nafasi ya meneja saba(07).

Bw.Kasase alisema kuwa nafasi hizi zimetangazwa kwa kufuata mpango mkakati wa GST wa mwaka 2010- 2015 ambapo kulingana na muundo wa taasisi nafasi hizo endapo zitafanikiwa kujazwa kulingana na idadi iliyotajwa zitakuwa zimekizi ikama ya mpango mkakati wa taasisi ulioanzishwa Disemba 9, 2005.

Kasase aliongeza kuwa matarajio makubwa baada ya ya mchakato kukamilika ni kwamba taasisi itaweza kukamilisha dira na dhima  kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na hapo awali kabla ya muundo kukamilika.

Kwa upande wa ushauri meneja utawala , alitoa wito kwa watumishi wa GST kufuata utaratibu , sheria na kanuni za mtumishi wa umma sababu ni njia pekee ya kufanikisha mpango wa matokeo makubwa sasa(BRN)

No comments:

Post a Comment