Mwanariadha wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius (kulia) akiwa na mpenzi wake, Reeva Steenkamp enzi za uhai wake.
Kesi ya mwanariadha wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius inaendelea leo siku ya nne mahakama kuu mjini
Pretoria, Afrika Kusini chini ya Jaji, Thokozile Masipa huku wakili wa Pistorious, Barry Roux akiendelea kujenga hoja kibao za kumtetea Pistorious.
Wakili huyo ambaye amekuwa mtetezi tangu mwanzo wa kesi ya Pistorious, amekuwa akigoma kusikia hata kifungo cha nje endapo Pistorious atahukumiwa.
Ameendelea kusisitiza kuwa mahakama inabidi imuangalie Pistorious zaidi kimatibabu endapo atahukumiwa kwenda jela kwani anavyoamini gerezani hakuna matibabu mazuri kwa mgonjwa kama yeye.
Pistorius alipatikana na kosa la mauaji bila kukusudia mwezi jana na huenda akakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 15 jela, lakini jaji anaweza kumpa kifungo cha nje au hata kumtoza tu faini.
GPL
No comments:
Post a Comment