Msanii Vichekesho maarufu kwa jina la Mzee Majuto Wekeend iliyopita alitakiwa kuwepo Dodoma kwenye ukumbi wa Matei lounge kwa ajili ya kufanya show, Sakata lilikuja pale mwandaaji wa show hiyo kunaswa akiwa analia, Picha lilianza pale ambapo Paparazi wetu alimnasa Dada huyo akiwa
chocho akinunguka kuwa kamtumia Mzee Majuto pesa Taslimu Shilingi laki tatu na nusu kwa ajili ya kuja kupush Mauzo ya CD yake, Ambapo aliwaalika mstaa kibao akiwemo Mzee Majuto,Asha Boko na wengine kibao.
Ilikuwa ni Majira sa nne Usiku ambapo wasanii wengine walikuwa wameshafika na alikuwa anasubiriwa Mzee majuto ili shughuli iweze kuanza lakini cha kushangaza mzee Majutokila akipigiwa simu anadai yupo Chalinze, Dada huyo aliendelea kulalamika kuwa mara ya nn hii kila nikipiga simu ananiambia nipo chalinze'' jamani sasa huu si usanii juu ya usanii, Pesa kachukua halafu anaharibu shugnuli ya watu sasa kama alikuwa hataki ni kwa nini kuchukua pesa ya watu? wasanii hembu jiheshimuni jamani acgeni kucheza na akili za watu.
Chanzo: Mtandao
Chanzo: Mtandao
No comments:
Post a Comment