Mkuu wa Wilaya ya Mbeya mjini Dr. Norman Sigela(mwenye suti nyeusi)pamoja na Mchezaji bora wa Mwezi wa Septemba wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara Anthony Matogolo wa timu ya Mbeya City(kushoto)wakionesha hundi yenye thamani ya Tsh Milioni 1/= kwa mashabiki wa timu yake mara baada ya kukabidhiwa rasmi na Mkuu wa wilaya hiyo kwa niaba ya wadhamini wakuu wa ligi kuu Vodacom Tanzania hapo jana kabla ya mechi kuanza baina ya timu Mbeya City na Azam FC,Ambapo Azam FC iliilaza Mbeya City kwa goli moja bila na anaeshuhudia kulia ni Katibu wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Mbeya(MREFU) Seleman Harub.
Mchezaji bora wa Mwezi wa Septemba wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara Anthony Matogolo wa timu ya Mbeya City akionesha kikombe chake.
mtanange ukiendelea katika ligi kuu ya vodakom katika
uwanja wa sokoine
Wachezaji wa timu ya Azam FC wakishangilia goli lao lililofungwa na Aggrey Morris katika mzunguko wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kati ya timu hiyo na Mbeya City hapo jana/juzi Azam FC iliilaza Mbeya City kwa goli 1-0.
No comments:
Post a Comment