Mwanamuziki
Mkongwe kutoka bendi ya muziki wa dansi ya Twanga Pepeta,pichani kulia
enzi za uhai wake akiwa kazini,ajulikanae kwa jina la Amigolas amefariki
Dunia usiku wa kuamkia leo,katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili
jijini Dar,Taarifa za awali ambazo chumba cha habari cha Globu ya Jamii
imezipata kutoka kwa vyanzo vya kuwaminika,zinaeleza kuwa Marehemu
Amigolas alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya Moyo mpaka kufariki
kwake.Tutaendelea kupeana taarifa zaidi kuhusiana na msiba huu kwa
kadiri zitakavyokuwa zikiingia.Mungu ailaze roho ya Marehemu mahala pema
peponi-Amin
No comments:
Post a Comment