Wayne Rooney yuko 'fiti' na ataanza kwa upande wa Manchester United dhidi ya Manchester City, lakini mshambuliaji Radamel Falcao hatocheza kutokana na kuwa bado majeruhi.
Meneja wa Man Utd Louis van Gaal amethibitisha kuwa nahodha wake atacheza baada ya kumaliza kutumikia adhabu yake, na kusema taarifa zinazodai kuwa ameumia si za ukweli.
Falcao hakucheza katika mechi dhidi ya Chelsea iliyomalizika kwa sare ya 1-1.
Winga Antonio Valencia naye amerejea baada ya kupona msuli wa paja.
Van Gaal ametupilia mbali taarifa zilizodai kuwa Rooney hana uhakika wa kucheza kwa sababu alionekana akichechemea katika shughuli moja ya wadhamini siku ya Jumatatu, Old Trafford.
No comments:
Post a Comment