Pages

Sunday, November 2, 2014

MANCHESTER UNITED YAPIGWA 1 - 0 DHIDI YA MANCHESTER CITY

Ligi kuu ya soka nchini England imeendelea hii leo kwa michezo miwili iliyopigwa huko jijini Manchester na jijini Birmingham .

Katika mchezo wa kwanza Mabingwa watetezi wa ligi hiyo Manchester City waliwafunga mahasimu wao wa jadi Manchester United kwa bao moja bila katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Etihad .

Bao pekee lililoamua mchezo huo lilifungwa na mshambuliaji raia wa Argentina Sergio Kun Aguerro ambaye alimalizia pasi ya Gael Clichy .

United katika mchezo huo ilimaliza ikiwa pungufu baada ya mlinzi Chris Smalling kuonyeshwa kadi nyekundu mapema kwenye kipindi cha kwanza .

Matatizo ya United hayakuishia hapo kwani baadaye mlinzi wa kimataifa wa Argentina Marco Rojo alilazimika kutolewa nje baada ya kuumia bega lake .

Huu ni ushindi wa nne mfululizo ambao City inaupata mbele ya United huku Sergio Aguerro akiendelea kuwaumiza mashetani wekundu akiwa amefunga mabao matano kwenye michezo sita dhidi ya United .


No comments:

Post a Comment