Hii ndio CD ya Saluti ambayo leo balozi wa Yesu kajikuta akiwapiga kikweli kweli Saluti Polisi Iringa
MWIMBAJI wa nyimbo za injili maarufu nchini Tanzania ambae ni mlemavu wa mkono mmoja Mwinjilisi Joseph Nyuki maarufu kwa jina la Balozi wa Yesu ajikuta mikonono wa polisi wakati akiendesha harambee yake ya Injili mtaa kwa Mtaa mjini Iringa.
Tukio hilo la balozi wa Yesu kukamatwa na polisi limetokea leo majira ya saa 8 mchana wakati gari la mwimbaji huyo wa Injili likipita katika mitaa mbali mbali ya mji wa Iringa kueneza injili kwa kuuza CD inayokwenda kwa jina la Saluti .
Mbali ya kuwa na kibali cha Manispaa ya Iringa kinachompa uhuru wa kueneeza injili kwa watu wote kupitia CD hiyo ya Saluti na kibali hicho kupitishwa polisi bado askari polisi walimfuata balozi huyo wa Yesu na kumtia nguvuni kuwa hapaswi kueneza injili kwa kupiga kelele mitaani.
Askari ambae jina lake halikuweza kunaswa mara moja alifika katika gari lenye namba za Usajili T 364 DPD ambalo lilikuwa limefunga muziki mnene na kupeperusha injili mtaani kiasi cha kila mmoja mjini hapa kuvutiwa na vionjo vya mwimbaji huyo na kulifuata gari hilo kununua CD kabla ya askari huyo kulipiga pini gari hilo eneo la Soko kuu Miyomboni mjini Iringa .
Baada ya kumsimaisha mwimbaji huyo kutoendelea na uuzaji wa CD hiyo askari huyo alimtaka kuonyesha kibali pamoja na kuzima muziki na kugeuza gari hilo kupeleka Polisi amri ambayo bila jeuri balozi wa Yesu alitii huku akisema ndio kazi ya kueneza injili hiyo ambayo kwake ameizoea .
Kwa upande wao wananchi ambao walikuwa wakinunua CD wameeleza kusikitishwa na hatua ya polisi kuzuia uenezaji wa injili huku kila siku mji wa Iringa watu wanapita na magari wakitangaza Ma Disco na matamasha yenye vichocheo vya maambukizi ya VVU huku wakiyafumbia macho.
Mtandao huu ulipofuatilia sakata hilo kituo cha polisi ulishuhudia suala hilo likiishia nje ya kituo cha polisi baada ya askari huyo kuyamaliza kiume na mwimbaji huyo nje ya kituo baada ya kuonyesha kibali halali cha Manispaa ya Iringa na wakati askari huyo akihoji zaidi juu ya kuzunguka kila kona likiwemo eneo hilo la polisi kwa kupiga muziki ghalfa Mungu alionyesha nguvu zake kufuatia gari jingine lililokuwa likiuza simu huku likipiga miziki ya duniani likipita nje ya kituo cha polisi bila kukamatwa ndipo askari kwa kuona hilo walimruhusu kuendelea na kazi ya kuitangaza injili.
Akizungumza na mtandao huu wa matukiodaima mara baada ya kuachiwa huru Balozi wa Yesu alisema kuwa polisi walifika na kumsimamisha na kumwomba kibali na baada ya kuonyesha aliachiwa huru na kuwa polisi wametimiza wajibu wao na kuwa hana kinyongo nao.
Pia alisema kuwa ziara yake mkoani Iringa na mikoa mbali mbali ni kuitangaza injili kupitia oparesheni yake ya Injili mtaa kwa Mtaa kwa watu wote waokoke na kuwa anaifanya hivyo kama njia ya kuuza CD yake baada ya kuchoshwa na unyonyaji unaofanywa na baadhi ya studio kwa kuwalalia waimbaji wa nyimbo za Injili nchini.
CHANZO:http://www.matukiodaima.co.tz/
|
No comments:
Post a Comment