Kamishna
Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(pichani) kesho tarehe 20
Machi, 2015 saa 8:00 mchana atawavisha vyeo Maafisa wa Jeshi la
Magereza wa ngazi mbalimbali wa Mkoa wa Dar es Salaam waliopandishwa
vyeo kwa mujibu wa Sheria.
Kwa
Mamlaka aliyopewa kisheria na Tume ya Polisi na Magereza ya Mwaka 1990,
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini atawavisha vyeo hivyo katika
Viwanja vya Chuo cha Maafisa wa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam.Tume
ya Polisi na Magereza katika Kikao chake Namba 2/2014/2015
kilichofanyika tarehe 16 Machi, 2015 chini ya Mwenyekiti Naibu Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Ame Silima(Mb) imewapandisha vyeo
Maafisa 292 wa ngazi mbalimbali kuanzia tarehe 16 Machi, 2015.Maafisa
hao waliopandishwa vyeo ni Mrakibu Mwandamizi wa Magereza kuwa Kamishna
Msaidizi wa Magereza 11, Mrakibu wa Magereza kuwa Mrakibu Mwandamizi wa
Magereza 41, Mrakibu Msaidizi wa Magereza kuwa Mrakibu wa Magereza 83
na Mkaguzi Msaidizi wa Magereza kuwa Mkaguzi wa Magereza 157.
Imetolewa na; Inspekta Lucas Mboje, Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
DAR ES SALAAM
19 Machi, 2015.
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
DAR ES SALAAM
19 Machi, 2015.
No comments:
Post a Comment