Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) leo limekamilisha upangaji wa ratiba ya mechi za robo fainali ya ligi ya mabingwa iliyofanyika katika mji wa Nyon, Switzerland.
Katika ratiba hiyo Real Madrid itacheza na Atletico Madrid huku Barcelona wao wakiwa na kibarua kigumu dhidi ya Paris Saint-Germain ama ‘PSG‘ ambayo iliiondoa Chelsea kwenye michuano hiyo.
FC Porto watakutana na Bayern Munich nao Juventus wakiwa na kibarua kikali dhidi ya AS Monaco ya Ufaransa iliyoiondoa Arsenal.
Mechi:
PSG Vs Barcelona
Atletico Madrid Vs Madrid
Porto Vs Bayern
Juve Vs Monaco
No comments:
Post a Comment