Pages

Monday, April 21, 2014

AJALI ILIYOTOKEA LEO ASUBUHI ILIYOUA WATU 20 BUSEGA MKOANI SIMIYU


basi lililopata ajali na kuua watu 20 leo asubuhi
WATU 20 wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa vibaya wilayani Busega Mkoani Simiyu leo asubuhi kufuatia ajali ya Bus la kampuni ya Luhuye iliyopasuka mpira, kuacha njia na kugonga nyumba.

Mbunge wa Jimbo la Busega ambaye pia ni Waziri wa uvuvi na maendeleo ya Mifugo Dakta Titus Kamani ameiambia Blog hii kwa njia ya Simu kwamba ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Sogesita wilayani humo.

Dakta Kamani amesema basi hilo lilikuwa likielekea Jijini Mwanza ndipo lilipopasua mpira wa mbele na kupinduka huku likigeukia lilikotoka kabla ya kuacha njia na kugonga nyumba kwenye kaya moja kijijini 
 
 iliyohusisha basi la abiria kampuni ya Luhuye T 410 AWQ lilokuwa likitokea Tarime Mkoani Mara likielekea Mkoani Mwanza.
Ajali hiyo imetokea jana majira ya saa 5:10 asubuhi barabara kuu ya mwanza – Mara katika kijiji cha Itwilima kata ya kiloleli wilaya ya Busega Mkoani Simiyu, ambapo watu wengine  wamejeruhiwa.Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Paschal Mabiti alisibitisha kutkea kwa ajali hiyo mbaya sana mmoja kati ya hao mwanamke aliyetambulika kwa jina la Lusia Wilson alifariki wakati akikimbizwa katika hospitali ya rufaa Bugando Jijini Mwanza.
Mabiti alieleza kuwa mama huyo aliyefariki wakati akikimbizwa katika hospitali ya rufaa Bugando aliacha watoto 3 ambao ni joyce Wilson (6), jenipha Wilson (3) na jack Wilson ambaye alikuwa na umri wa miezi 2, huku akieleza majeruhi wote walikimbizwa katika hospitali ya Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza.

No comments:

Post a Comment