Shirikisho
la Mchezo wa Bao Tanzania limelaani vikali wanasiasa wanao simama na
kutoa maneno ya kejeli zidi ya waasisi wa Muungano wa Tanzania Bara na
Visiwani kwani huko ni kutokuwa na maadili yenye sura alisi ya
Utanzania.
Hayo
yamesemwa na Raisi wa shirikisho hilo Bw Monday Likwepa kwenye
Mashindano ya Mchezo maalum wa Bao wa Maadhimisho ya Miaka 50 ya
Muungano wa Tanzania Bara na Visiwani yanayo fanyika Makumbusho na
Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
"Shirikisho kwa kupitia mchezo huu na wadau wake wote wamesikitishwa na
kukerwa sana na tunalaani vikali vitendo vya baadhi ya Wajumbe wa Bunge
maalum la Katiba na Wabunge wa Jamuuri ya Muungano kwa kutumia nafasi
walizo pewa sasa wamegeuza na kuwatuhumu, zalilisha na kuwakashfu
waasisi wa Muungano wetu Hayati Baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere na Mzee
Abeid Amani Karume’’ Alisema Bw Likwepa.
No comments:
Post a Comment