Kiungo
wa Yanga, Frank Domayo, akisaini mkataba wa kujiunga na Azam, katika
msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, wakati akiwa kambi ya timu ya Taifa jijini
Mbeya leo jioni.
Habari
zilizoufikia mtandao huu zinasema kuwa Viongozi wa Azam,
wamebambwa jijini Mbeya wakati wakiwa katika harakati za kumsainisha
kiungo huyo ambapo walifanikiwa kunasa dole gumba pekee kabla ya kunasa
saini yake.
Zoezi
hilo lilishitukiwa na Viongozi wa timu ya Taifa ambao wapo jijini Mbeya
na timu ya Taifa Kambini, ambapo lilishatolewa tamko kuwa hakuna Klabu
yeyote inayoruhusiwa kutinnga katika kambi ya Taifa kwa lengo la kuwania
wachezaji ili kuwasainisha kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu.
Aidha
imeelezwa kuwa Kiungo huyo tayari alishafanikiwa kuweka saini ya dole
gumba kwa mkataba wa kuitumikia Klabu hiyo ya mabingwa wapya wa ligi Kuu
Bara Azam Fc miaka miwili.
Mtonyaji wa habari hizi kutoka jijini Mbeya, ametonya kuwa Viongozi hao wamenaswa jioni ya leo wakati wakifanya jaribio hilo.
Hata
hivyo zoezi hilo la usajili wa Domayo halikuweza kukamilika baada ya
Polisi kuingilia kati na kuwatimua viongozi wa Azam, ambao walitinga
Kambini hapo bila kufuata utaratibu.
Na
kwa tukio hilo askari walilazimika kuwakumbusha viongozi hao kuwa
tayari Rais wa TFF, Jamal Malinzi, alisha toa tamko kuwa hatoruhusiwa
kiongozi yeyote wa timu kuvamia kambi ya Taifa kwa lengo la kuwarubuni
wachezaji na kuwasainisha.
Kwa
mujibu wa Mshauri wa Rais Pelegrinius rutayungwa, aliyeko Jijini Mbeya,
amesema kuwa Azam tayari wamekiuka na kuvunja Amri ya Rais wa TFF, na
kuongeza kuwa suala hilo litafikishwa katika Kamati ya Maadili ili
kujadiliwa.
Aidha aliongeza kuwa tayari mikataba ya Domayo kwenda Azam, wanayo mkononi huku ikiwa na Dole gumba pekee bila saini.
Domayo
amesaini Azam FC baada ya kumaliza Mkataba wake wa miaka miwili na
Yanga SC, ambayo alijiunga nayo akitokea JKT Ruvu miaka miwi iliyopita.
Katibu
wa Azam FC, Nassor Idrisa Mohamed ‘Father’ amesema katika kuendelea
kukiimarisha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao wamepiga hatua nyingine
kwa kumsaini Domayo baada ya jana kumnasa Didier Kavumbagu wote wa
Yanga.
“Kama
unavyojua, baada ya kumaliza msimu vizuri tukiwa mabingwa wa Bara,
tuligundua mapungufu kwenye kikosi chetu na kwa ushauri wa mwalimu wetu
(Joseph Marius Omog) ndiyo tunayafanyia kazi,”alisema Father.
Domayo
anakuwa mchezaji wa wa pili ndani ya siku mbili kusajiliwa na Azam FC
kutoka kwa mabingwa wa zamani na mabingwa wa kihistoria Tanzania Bara,
Yanga SC baada ya jana klabu hiyo kumsainisha mshambuliaji Mrundi Didier
Kavumbagu.
No comments:
Post a Comment