Mwenyekiti
mwenza wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikiendesha
Kikao cha Kamati hiyo kilichokutana katika Ukumbi wa Wizara ya Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa { TAMISEMI }
Mjini Dodoma.
Baadhi
ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambao ni Wajumbe wa
KamatiI Kuu ya Taifa ya Sensa Tanzania wakiendelea na Kikao chao Mjini
Dodoma. Kutoka
Kulia ni Waziri wa Habari M,h. Said Ali Mbarouk, Waziri wa Uwezeshaji
Wananchi Kiuchumi Mh. Zainab Mohd, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala
za Mikoa na Idara Maalum Mh. Haji Omar KLheir pamoja na Waziri wa Nchi
Ofiisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Mwinyihaji
Makame.
Baadhi
ya Wajumbe wa Kamati Kuu ya Sensa kutoka Kushoto ni Kamishna wa Sensa
Tanzania Bara Hajat Amina Mrisho Naibu Waziri wa Fedha wa Serikali ya
Muungano wa Tanzania Mh. Muigulu Nchemba na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu Dr. Florens Turuka.
Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania Dr. Alina Chua akitoa
Taarifa fupi juu ya uhakiki wa mipaka kwa baadhi ya Wilaya Nchini
Tanzania. Kushoto ni Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Nd. Mohd Hafidh.
Kamati Kuu
ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 inatarajia
kuzindua Chapisho la Tatu la Taarifa za msingi za Kidemografia, Kijamii
na Kiuchumi Tarehe 23 April mwak huu wa 2014 katika kusherehekea miaka
50 ya Muungano wa Tannganyika na Zanzibar.
Uzinduzi
huo unaotarajiwa kufanywa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Dr. Jakaya Mrisho Kikwete utafanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa
Julius Nyerere Mjini Dar es salaam.
Taarifa
ya uzinduzi huo imefahamika ndani ya Kikao cha Kamati Kuu ya Taifa ya
Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 kilichofanyika chini ya Mwenyekiti
Mwenza wa Kamati hiyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
Ali Iddi kwenye ukumbi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa iliyopo Mjini Dodoma.
Akitoa
Taarifa ya Wizara ya Fedha ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mh. Muigulu Nchemba alisema
maandalizi ya machapisho mengine 10 yanaendelea kufuatia kukamilika kwa
zoezi la Sensa ya Watu lililofanyika mwezi Oktoba mwaka 2012 Nchini kote
Tanzania.
Mh.
Nchemba aliyataja baadhi ya machapisho hayo yatazingatia zaidi takwimu
zilizokusanywa na wataalamu wa Sensa zinazohusu Vizazi na ndoa, Elimu,
Uhamiaji na Makazi pamoja na hali ya ulemavu.
Alizipongeza
Taasisi na Mashirika ya Kitaifa na Kimataifa kupitia Walaamu wao kwa
kushirikiana na Wizara hiyo katika kufanikisha kazi ya Sensa licha ya
changamoto kubwa za upatikanaji wa fedha.
“
Tunawashukuru wadau wetu wa maendeleo ambao kwa kweli wametusaidia
kutuunga mkono katika zoezi hilo na zaidi ya Shilindi Bilioni Tatu
{3,000,000,000 } walizitenga kwa ajili ya kazi hiyo “. Alisema Mh.
Muigulu Nchemba.
Akitoa
Taarifa fupi ya utekelezaji wa kazi ya uhakiki wa Baadhi ya mipaka ya
Wilaya Tanzania Bara na Zanzibar kwenye Kikao hicho Mkurugenzi Mkuu wa
Ofisi ya Taifa yaTakwimu Tanzania Dr. Albina Chua alisema zoezi la
uhakiki huo tayari limeshafanyika kwa Wilaya za Gairo na Chemba kwa
Tanzania Bara na Wete na Micheweni kwa upande wa Zanzibar.
Dr.
Albina alisema uhakiki huo wa mipaka ya Wilaya na Halmashauri umekuja
kufuatia mapungufu yaliyojitokeza katika baadhi ya Wilaya hizo na
kusababisha kuwemo kwa matumizi ya mipaka zaidi ya mmoja.
Alisema
Utekelezaji wa kazi hiyo ulitokana na matokeo ya kazi ya awali
iliyofanywa katika Wilaya ya Gairo ambapo Kamati ya Taifa ya ushauri ya
Sensa iliagiza kufanyika kama sampuli ya kujua tatizo la utoaji wa
mipaka ya kiutawala.
Naye
Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mohd Hafidh akitoa
Taarifa ya Utekelezaji wa Kazi hiyo ya uhakiki wa mipaka kwa upande wa
Zanzibar alisema kazi hiyo imeanza kwa kuundwa kwa Timu ya Maofisa
watakaoshughulikia kazi hiyo.
Alisema
kazi hiyo iliyoanza Tarehe 8 Aprili mwaka huu inatyarajiwa kuchukuwa
wiki mbili katika Wilaya ya Wete na kuendelea katika Wilaya ya Micheweni
lengo ni kuziwezesha Taasisi husika kujua changamoto mbali mbali za
mipaka ya Wilaya na namna ya kuzitafutia ufumbuzi ili kuwa na Mipaka
inayofanana.
Akitoa
shukrani zake kwa Wajumbe wa Kamati hiyo Mwenyekiti Mwenza wa Kamati
Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliipongeza Sekreteri ya Kamati
Kuu ya Taifa ya Sensa kwa Kazi kubwa inayoendelea kuifanya tokea
kumalizika kwa zoezi la Sensa ya watu na Makazi Nchini Tanzania.
No comments:
Post a Comment