Mwandishi
wa kitabu kinachoelezea namna watanzania na makampuni ya usambazaji ya
hapa Tanzania yanavyoweza kushiriki, kuwezeshwa na kunufaika na sekta ya
nishati ya gesi asilia, Bi. Neema Lugangilra Apson, akielezea maudhui ya Kitabu chake kwa wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho uliofanyika jana usiku jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof.
Elisante Ole Gabriel (kushoto) akiteta Jambo na Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi Ombeni Sefue jana wakati wa uzindizi wa kitabu cha “Local Content
in Supplier Development” kilichoandikwa na Neema Lugangilra Apson.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof.
Elisante Ole Gabriel (kushoto) akiteta Jambo na Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi Ombeni Sefue jana wakati wa uzindizi wa kitabu cha “Local Content
in Supplier Development” kilichoandikwa na Neema Lugangilra Apson
Bi.
Neema Lugangilra Apson akionesha kitabu chake kinachoitwa “Local
Content in Supplier Development” kinachoelezea namna watanzania na
makampuni ya usambazaji yanavyoweza kushiriki, kuwezeshwa na kunufaika
na sekta ya nishati ya gesi asilia hapa.
Mgeni
Rasmi Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akikata utepe kuashiria
uzinduzi wa kitabu kinachoeleza namna watanzania na makampuni ya
usambazaji yanavyoweza kushiriki, kuwezeshwa na kunufaika na sekta ya
nishati ya gesi asilia hapa. Kulia ni mwandishi wa kitabu hicho Bi. Neema Lugangilra Apson.
Mgeni
Rasmi Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akipokea kitabu
kinachoelezea namna watanzania wanavyoweza kushiriki na kunufaika na
sekta ya nishati ya gesi asilia hapa nchini. Kulia ni mwandishi wa
kitabu hicho Bi. Neema Lugangilra Apson.
Neema Lugangilra Apson akimkabidhi Binti yake Georgia Blessings Apson kitabu
alichokiandika kinachoelezea namna watanzania na makampuni ya
usambazaji yanavyoweza kushiriki, kuwezeshwa na kunufaika na sekta ya
nishati ya gesi asilia hapa.
Msemaji
wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Assah Mwambene (katikati)
akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kushoto)
wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Local Content in Supplier Development
kilichoandikwa na Bi. Neema Lugangilra Apson jana Jijini Dar es Salaam,
kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa magazeti ya serikali (TSN) Gabriel
Nderumaki.
**************************************************
SERIKALI
imewasisitiza wananchi hususan wafanyabiashara kote nchini kuwekeza
katika utoaji wa huduma mbalimbali za kijamii katika maeneo yote yenye
miradi ya gesi nchini.
Kauli
hiyo imetolewa jana usiku jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya uzinduzi wa kitabu
kilichoandikwa na mtanzania Bi. Neema Lugangira Apson chenye maudhui ya
namna Kampuni za Kitanzania zilizojikita katika uwekezaji wa gesi
zinavyoweza kushiriki ,kuendelezwa katika uwekezaji wa sekta ya gesi
asilia nchini.
Akizungumza
katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali,
balozi, makampuni yaliyowekeza katika sekta ya gesi na wadau mbalimbali
Balozi Sefue amesema sekta ya gesi ni moja eneo lililo na fursa nyingi
za uwekezaji kwa watanzania.
Amesema
ni wakati wa wananchi kuziona fursa hizo na kuwekeza katika maeneo yote
yanayohitaji uwekezaji wa huduma mbalimbali hususan za usambazaji na
uuzaji wa vyakula, ujenzi wa nyumba za kulala wageni, uuzaji wa bidhaa
muhimu, uuzaji wa bidhaa na vifaa vya gesi pamoja na vitu vingine
vinavyohitajika katika maeneo ya miradi.
Ameeleza
kuwa serikali imejipanga vizuri katika kuhakikisha kuwa sekta ya gesi
inasimamiwa na kuendelezwa vizuri kisera na kufafanua kuwa tayari hatua
mbalimbali zimekwisha chukuliwa kuhakikisha kuwa sekta ya gesi inakuwa
na manufaa kwa wananchi na ustawi wa taifa.
“Katika hili serikali
tumejipanga vizuri kwa kuhakikisha sekta hii inaleta manufaa kwa taifa,
tumejifunza kupitia uzoefu mkubwa walioupata wenzetu hasa nchi kubwa
zilizopiga hatua katika sekta ya gesi” Amesisitiza Balozi Sefue.
Balozi
Sefue amewataka wafanyabiashara na wasambazaji wa ndani walioingia
kwenye sekta ya nishati ya gesi na mafuta kufanya kazi zao kwa weledi
mkubwa na kuzingatia ubora na viwango vinavyokubalika ndani na nje ya
nchi na kuwasisitiza kuendelea kujifunza zaidi na kutafuta masoko ya
bidhaa wanazozalisha ili kujenga uchumi imara.
Amesema
serikali inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wanaowekeza katika
sekta ya gesi na utafutaji wa mafuta nchini na kutoa wito kwa makampuni
yanayojihusisha na sekta ya gesi kushirikiana na serikali katika mpango
wa kuhakikisha shughuli wanazozifanya zinaboresha maisha ya watanzania.
Akizungumzia
uzinduzi wa kitabu hicho Balozi Sefue amesema kuwa kitabu hicho kina
mchango muhimu sana katika uendelezaji wa sekta ya gesi hapa nchini na
kufafanua kuwa elimu iliyomo ndani ya kitabu hicho ni kwa manufaa ya
watanzania wote.
Kwa
upande wake mwandishi wa Kitabu hicho Bi. Neema Lugangira Apson
akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu chake amesema kuwa ameamua
kuandika kitabu hicho kutokana na unyeti wa sekta ya Gesi asilia na
umuhimu wa mchango wake kwa maendeleo ya taifa.
Amesema kitabu hicho
kitachangia kuongeza uelewa wa masuala ya gesi kwa wananchi na makampuni
ya kitanzania yanayowekeza katika sekta ya gesi kutokana changamoto
iliyopo ya uelewa mdogo juu ya sekta hiyo jambo linalochangia ushiriki
mdogo.
“Nimeandika
kitabu hiki kutoa mchango wangu kuelezea namna kampuni za kitanzania
zinavyoweza kushiriki kikamilifu na kuendelezwa ili zilete manufaa kwa
watanzania, ugunduzi wa gesi umekuja wakati ambao watanzania tulio wengi
hatujajiandaa vizuri na si kwamba hatuwezi katika hili jambo la msingi
ni sisi wenyewe kuweka utashi na utayari wa kunufaika ” Amesisitiza.
Ametoa wito kwa
makampuni ya ndani yanayojihusisha na sekta ya gesi kuungana uwekezaji
yaweze kuwa na nguvu ya kushindana na makampuni kutoka nje ya nchi.
“Ni
lazima tuhakikishe kuwa tunaimarisha makampuni yetu ya ndani ili tuweze
kushindana na makampuni ya nje ikiwezekana mamlaka husika zitoe motisha
kwa makampuni au wafanyakazi wanaofanya vizuri na wale wasiofanya
vizuri waadhibiwe” Amesisitiza Bi. Neema.
Aidha
amesema kitabu hicho kitapatikana bure ikiwa ni sehemu ya mchango wake
kutoa maarifa kwa watanzania na wadau wote wa sekta ya gesi na kuongeza
kuwa utaratibu wa kukichapisha kitabu hicho ambacho sasa kipo kwa lugha
ya kiingereza unafanyika ili kiweze kupatikana kwa lugha ya Kiswahili.
Naye Balozi
wa Uingereza nchini Tanzania ambaye ubalozi wake umehusika kutoa
mchango wa ufanikishaji wa kitabu hicho Bi. Diane Melrose amemsifu
mwandishi wa kitabu hicho na kueleza kuwa uzinduzi wa kitabu hicho ni
fursa pekee ya wadau mbalimbali kujifunza mengi kuhusiana na sekta ya
gesi nchini.
Amesema
Tanzania na Uingereza zimekuwa na uhusiano wa karibu katika utekelezaji
wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kuongeza kuwa nchi yake itaendelea
kushirikiana na Tanzania katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya
maendeleo kwa wanufaa ya wananchi.
Katika
hatua nyingine mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Wachimba Madini Nchini
(TPSF) Bw. Richard Kasesela akizungumza katika uzinduzi huo ameeleza
kuwa kitabu hicho kitasaidia kuboresha sera zinazosimamia sekta hiyo
hapa nchini.
Kuhusu
sekta ya gesi nchini amesema kuwa wapo baadhi ya watu wamekuwa na
mitazamo hasi juu kuhusu manufaa ya gesi kwa uchumi wa Tanzania ambao
huilaumu serikali kwa kueleza kuwa gesi na mafuta havina mchango wowote
kwa uchumi wa Tanzania jambo ambalo halina ukweli wowote kutokana na
juhudi kubwa inayofanywa na serikali kuhakikisha sekta hiyo
inawanufaisha watanzania.
No comments:
Post a Comment