Shomari Kapombe (kulia) akiwa mazoezini na timu ya Azam, kushoto ni John Boko
Dar es Salaam Baada ya kuwapo kwa taarifa za uhakika za beki Shomari Kapombe kujiunga Azam FC, kocha wa zamani wa Taifa Stars ametetea uamuzi wa mchezaji huyo kuwa amefanya uamuzi sahihi na muda mwafaka.
Kapombe anadaiwa kumalizana na Azam kwa ajili ya
kuichezea msimu ujao wa Ligi Kuu na tayari ameanza kujifua na kikosi cha
timu hiyo chenye maskani yake katika eneo la Chamazi lililoko pembezoni
mwa Jiji la Dar es Salaam.
Kabla ya kuhamia Azam, Kapombe alikuwa anacheza
soka ya kulipwa katika klabu ya AS Cannes ya Ufaransa aliyojiunga nayo
akitokea Simba SC kabla ya hivi karibuni kuamua kuvunja mkataba.
Akizungumza na gazeti hili, Msola alisema anaunga mkono uamuzi huo wa Kapombe kwavile anaamini Azam ni timu pekee inayoweza kuendeleza kipaji cha mchezaji huyo.
“Niseme wazi uamuzi wa Kapombe kujiunga na Azam ni
sahihi kabisa ukizingatia kwa umri wake ndiyo timu ambayo anaweza
akacheza bila presha za mashabiki na kufikia malengo yake.
“Nilimshauri aangalie maisha yake kwa sababu hizo
timu mbili (Simba na Yanga) zina mambo mengi isitoshe hana elimu ya
kutosha hivyo ni lazima awe makini kutumia kipaji chake ili baadaye
asiye akajutia,” alisema Msola.
”Nimekuwa nikimpa ushauri kila wakati kama ambavyo
amekuwa akipewa na Profesa Madundo Mtambo, hivyo nina uhakika anapita
njia sahihi na atafanikiwa.”
No comments:
Post a Comment