Wananchi wa mji wa Dodoma wakiangalia sehemu ya madhara ya tukio
la moto uliotokea usiku wa kuamkia leo katika baadhi ya maduka yaliopo
kwenye Barabara ya Nyerere Karibu na Makao makuu ya CCM mjini
Dodoma,moto huo umeteketeza maduka matatu na mgahawa wa New Chick Villa
Reustaurant.
Maduka yaliyoathirika na moto huo ni Gulio La Mahafa Duka lililokuwa linauza bidhaa mbali mbali kwa jumla na reja reja zikiwamo bidhaa za Bakhresa,Duka la Esheki Investment lililo kuwa likiuza bidhaa za maofisini,vitabu na huduma ya uchapaji pomoja na Duka la madawa la lijulikanalo kama Kavula Pharmacy.
Wakazi wa Mji wa Dodoma wakiendelea kuangalia maduka hayo huku wengi wakiwa hawaamini kilichotokea.
Sehemu iliyokuwa na maduka ikiwa imeteketea kabisa kwa moto
uliotokea leo Barabara ya Nyerere karibu na Ofisi za makao makuu ya
Chama cha Mapinduzi CCM.
No comments:
Post a Comment