Majirani wakimuhudumia majeruhi
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la London Haonga(61)
mkazi wa Kijiji cha Mapogolo Kata ya Mbebe Wilaya ya Ileje Mkoani Mbeya amejeruhiwa
vibaya kwa kukatwa nyeti zake na watu watatu wasiofahamika kisha kutokomea nazo
kusikojulikana.
Tukio
hilo limetokea majira ya saa mbili usiku April 19 mwaka huu baada ya mmoja kati
ya watuhmiwa kufika nyumbani kwa mzee huyo kisha kubisha mlango akiomba msaada
wa kuonyeshwa njia akidai amepotea njia.
Mzee
London alipotoka nje ya nyumba akiwa anamwelekeza njia mtu huyo anayedaiwa
kuwani mjukukuu wake mita chache kutoka nyumbani kwake alifunikwa na kitambaa
usoni na watu wawili kisha kuangushwa na kukatwa nyeti zake ambazo waliondoka
nazo.
Mtendaji
wa Kijiji cha Mapogolo Cosmas Haonga amesema baada ya unyama huo Mzee London
alipoteza fahamu na alipozinduka alipiga yowe kuomba msaada ambapo majirani
walifika na kutoa msaada wa kumkimbiza Hospitali ya Wilaya ya Ileje huku
wakiwasaka watuhumiwa wa tukio hilo.
Kwa
mujibu wa Mtendaji wa Kijiji imedaiwa kuwa watuhumiwa wa tukio hilo wanatokea
Mpemba wilaya ya Momba ambao walitambuliwa na mhanga wa tukio hilo ambapo baada
ya kupewa PF 3 mzee London amekimbizwa Hospitali ya Rufaa Mbeya ambapo
alifikishwa Hospitali ya Rufaa majira ya saa 11:00 jioni April 20 huku
akilalamika kwa maumivu makali.
Kwa
upande wake Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi amethibitisha kutokea
kwa tukio hilo na kudai kuwa chanzo cha awali imedaiwa sababu za kutendewa
ukatili huo umetokana na mmoja wa ndugu aliyedai kuwa mzee huyo anatuhumiwa
kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wa mdogo wake hivyo watu hao walitumwa
kwa nia ya kulipiza kisasi.
Aidha
imedaiwa kuwa baadhi ya viungo vimekamatwa na wengine kudai kuwa tukio hilo
kuhusishwa na imani za kishirikina kwani imedaiwa watuhumiwa kuimbilia nchi
jirani mara baada ya kutenda kitendo hicho cha kikatili.
Kamanda
Msangi ameoa wito kwa jamii kuacha tabia za kujichukulia sheria mkononi amesema
pindi wanapokuwa na migogoro ni vema kutatua migogoro kwa njia ya mazungumzo
ili kuleta amani na kuahidi wale wote waliohusika na tukio hili wanakamatwa na
kufikishwa kwenye mikono ya sheria kwani hakuna mtu aliye juu ya sheria.
|
No comments:
Post a Comment