Pages

Friday, April 4, 2014

PICHA MBALI MBALI ZA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DR. ALI MOHAMED SHEIN ALIPOTEMBELEA SEHEMU MBALI MBALI HUKO ZANZIBAR.









Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa ZSSF Abduwakil Haji Hafidh,(kushoto) wakati alipotoa maelezo ya ramani ya kiwanja cha Mapembea Kariakoo Mjini Unguja,alipofika kuangalia maendeleo ya ujenzi wa kiwanja hicho.



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akitoa maelekezo
kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali maalim Abdalla Mzee wakati alipoitembelea Skuli ya Lumumba Mjini Unguja leo,baada ya kutoa agizo kuondoshwa Gereji ya magari waliovamia eneo la Skuli hiyo,(kulia) Msaidizi Mwalimu Mkuu Taaluma Bimkubwa Ali Mohamed,na (kushoto) Katibu Mkuu Bi Mwanaidi Saleh.


Uwanja wa mapembea wa Kariakoo Mjini Unguja ukiwa katika hatua za mwisho
Uwanja wa mapembea wa Kariakoo Mjini Unguja ukiwa katika hatua za mwisho katika
matengenezo,ambapo Rais wa wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, aliahidiwa kumalizika hivi karibuni wakati alipofanya ziara ya kuona maendeleo ya ujenzi huo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, atembelea maendeleo ya Ujenzi wa Mnara wa Kumbu kumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar unaojengwa katika viwanja wa Kisonge Michenzani Mjini Unguja. (Picha zote - Ikulu Zanzibar)
   

No comments:

Post a Comment