Mtangazaji wa MKASI TV Salama Jabir kupitia page yake ya instagram @ecejay amepost picha ya mastaa kadhaa wa bongo wakiwemo wasanii D-Knob, Godzilla Producer Marco Chali na wengine wakiungana na wabongo kama Mbunge Zitto Kabwe na wengine duniani kupinga ubaguzi wa mchezaji wa Barcelona Dani Alves wa kutupiwa ndizi uwanjani.
Mh.Zitto Kabwe
Club ya Villareal imeamua kumfungia maisha yule shabiki ambae alionyesha kitendo hicho cha kibaguzi kwa kumrushia ndizi Dani Alves, kitendo ambacho kilitafsiriwa kwa Alves kufananishwa na nyani.
Wachezaji kadhaa wamemsupport kwa ujasiri wake wa haraka na kula
ndizi hiyo aliyotupiwa uwanjani alafu akaendelea na game.
Mwingine alieonyesha support ni Samuel Eto’o ambae baada ya kuweka
picha zake mbili akiwa kwenye magari yake ya kifahari na kuandika
‘samahani nilisahau kuuliza, kuna yeyote anataka kuwa nyani kama mimi?’
No comments:
Post a Comment