Kutokana
na mjadala wa bajeti ya wizara ya mambo ya nje uliokuwa unaendelea ,
Mbunge wa Nkasi Ndugu Ali Kessy ameporomosha matusi mazito kwa
wazanzibar kuwa ni watu wa hovyo na ambao kila mara wanalialia tu kuwa
wanabaguliwa , wanadai mambo mengi kuliko uwezo wao na wakati
hawachangii hata senti kwenye Muungano na hivyo kama wanaona wanaonewa
waende kwenye nchi yao sio kukaa kwetu..
Alienda
mbali zaidi kusema kuwa Zanzibar Majimbo ya uchaguzi ni madogo kiasi
kwamba ukipigania filimbi wananchi wote wanakusanyika ila bado wanapewa
fedha za mfuko wa Jimbo jambo ambalo sio haki , na pia hata umeme
hawalipi na maji pia .
jambo
hili lilimfanya mbunge wa CCM ndugu Chombo , kuomba muongozo na Kumtaka
naibu Spika a mwambie Kessy kamwe asikanyage Zanzibar , hii ilikuwa
baada ya kumuita mwendawazimu , na alisema ni bahati mbaya kwa CCM kuwa
na mbunge mwendawazimu kama huyu ....!
No comments:
Post a Comment