KAMATI ya Uchaguzi ya klabu ya Simba, chini ya Mwenyekiti
wake Damas Ndumbaro, imempiga chini Mgombea wa nafasi ya Urais, Michael Richard
Wambura, hatua iliyomuweka katika mtego wa kuendelea na nia yake ya kuwa Rais wa Simba.
Michael Wambura
Akizungumza
na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Ndumbaro
alisema kuwa Wambura haruhusiwi kugombea Simba kwasababu ya kosa la
kimaadili, ila anaweza kukata rufaa kwa Kamati ya Maadili ya Shirikisho
la Soka nchini (TFF).
Swed Mkwabi
Naye
Swed Mkwabi, amepita katika pingamizi alilowekewa katika mbio hizo cha
Uchaguzi mkuu wa Simba utakaofanyika Juni 29. Mkwabi anawania nafasi ya
Makamu wa Rais, nafasi ambayo imekuwa ngumu, ingawa mwenye anajiamini
kuwa anayo sababu ya kuwa bosi wa Simba kutokana na kuungwa mkono na
wanachama wengi.
No comments:
Post a Comment