Pages

Wednesday, May 28, 2014

MMILIKI WA MANCHESTER UNITED AMEFARIKI



Mmiliki wa Klabu ya Manchester United Malcolm Glazer amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 85.

Familia ya Glazer ilinunua Manchester United kwa paundi milioni 790 mwaka 2005 licha ya mashabiki kupinga hatua hiyo.

Baada ya hapo United walishinda kombe la EPL mara tano - 2005, 2008, 2009, 2011 na 2013, na pia Champions League mwaka 2008.

Glazer ambaye ni Mmarekani pia alinunua klabu ya NFL ya Tampa Bay Buccaneers mwaka 1995.

No comments:

Post a Comment