Meneja
Ustawi wa Jamii na Uhusiano wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu
Muhimbili (MOI) Bw. Jumaa Almasi (katikati) akiwaeleza waandishi wa habari
(hawapo pichani) kuhusu hatua iliyofikiwa katika kupanua huduma za Taasisi hiyo
ikiwemo kukamilika kwa jengo jipya la kisasa litakalokuwa na vifaa vya kisasa
kama MRI ( magnetic Resonance Imaging) CT-SCAN (Computerized Tomography).kushoto
ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Bi Fatma Salum na kulia ni Afisa
uhusiano wa Taasisi hiyo Bw. Patrick Mvungi.
Muonekano
wa Jengo jipya la Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu Muhimbili
(MOI) ambalo linatarajiwa kukamilika mapema mwaka huu,kukamilika kwa jengo hilo
kutasaidia Taasisi hiyo kupanua huduma zake na kupunguza idadi ya wagonjwa
wanaoenda kutibiwa nje ya nchi kwa kwa asilimia 80 ikiwa ni juhudi za Serikali
kuboresha huduma za Afya hapa nchini. Picha zote
na Idara ya Habari Maelezo
P.O. Box 65474; DAR ES SALAAM,
TANZANIA,
MUHIMBILI COMPLEX
Executive
Director: +255-022-2153359
General lines:
+255-022-2151298/2152937/2152938
FAX: +255-022-2151744: E-Mail: info@moi.ac.tz: Website: www.moi.ac.tz
OFFERING
SERVICES IN ORTHOPAEDICS, NEUROSURGERY AND TRAUMATOLOGY
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
Mradi wa jengo jipya la MOI, (MOI Phase III) ambao utagharimu zaidi
ya Tshs billion 30 utaisaidia serikali kupunguza gharama za rufaa za kuwapeleka
wagonjwa nje ya nchi kufuata huduma kutokana na
baadhi ya huduma na vipimo kutokuwepo nchini,rufaa hizo huwa ni za gharama kubwa sana
Mradi huo utaiwezesha
MOI Kuwa na vifaa vya kisasa vya MRI (Magnetic Resonance Imaging), CT-SCAN
(Computerized Tomography) ambavyo vichache sana hapa nchini na Cyberknife digital
angiography (DSA) ambacho hakipo kabisa Tanzania
MOI itaweza kuwa na vitanda 20 vya wagonjwa
mahututi kutoka 8 vilivyopo sasa,wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum
(high dependence ward ) vitanda 24 ambayo haipo kwa sasa,wodi ya wagonjwa wa
kuchangia huduma (cost sharing) zikiwa na jumla ya vitanda 240 na wodi za
wogonjwa wa kulipia 62 na kuifanya taasisi kuwa na vitanda 380 kutoka 159
vilivyopo na hivyo kuondokana na adha ya wagonjwa kurundikana wodini na kulala
kwenye magodoro chini
Aidha,mradi utatoa
fursa ya Ajira 243 kwa watanzania katika kada za udaktari,uuguzi,wauguzi
wasaidizi na kada nyingine ambazo zimeainishwa kutokana na mahitaji
Huduma nyingine ni uanzishwaji
wa mfumo “paperless system” ambao unahusisha utoaji wa huduma kwa kutumia mfumo
wa kieletroniki zaidi na kuachana na mfumo wa sasa wa kutumia Mafaili ya
makaratasi mengi na unafanya wagonjwa watumie muda mwingi kabla ya kupata
huduma
Taasisi ya MOI inawaasa
watanzania kuachana na kasumba ya kukimbilia kupata matibabu nje ya nchi kwa
magonjwa yanayoweza kutibika hapa nchini ambapo wanatumia gharama kubwa wakati
huduma hizo zinapatikana hapa nchini kwa gharama nafuu
IMETOLEWA
NA
MKURUGENZI
MTENDAJI
TAASISI
YA TIBA YA MIFUPA MOI
No comments:
Post a Comment