Mashabiki
wa Timu ya simba wakijikusanya nje ya jengo la klabu hiyo kongwe
kupinga wambura kuondolewa kwenye uchaguzi unakuja hivi karibuni.
Hapa mashabiki wakizidi kujikusanya kwa wingi mchana huu
Wanachama
wa simba wakiwa wamelizunguka Jengo la klabu yao mchana huu kupinga
kuondolewa kwa wambura kwenye uchaguzi wa klabu hiyo
Wanachama
wa Simba wakipiga kelele nje ya jengo la klabu yao hiyo wakitaka wapewe
ufafanuzi wa kina kwanini wambura ametolewa kwenye uchaguzi unaokuja
Mmoja
wa wanachama wa Simba akiongea na mamia ya wanachama nje ya jengo la
klabu hiyo kutaka wambura arejeshwe mara moja kwenye orodha ya wagombea
Hapo mmoja ya wanachama waliojikusnya akiwatuliza wanachama wenzake ili waweze kupatamaelezo
Polisi
wakiwa wamefika eneo la klabu ya simba ili kuimarisha ulinzi na
kuwataka wanachama wa simba kutulia ili wapate majibu kwa kamati ya
uchaguzi
Mamia ya wanachama wa simba wakiwa nje ya jengo la simba mchana huu
Mamia
ya wapenzi na washabiki wa klabu kongwe ya mpira wa miguu hapa nchini
Simba leo mchana wamejikusanya kwa wingi na kupinga Michael Wambura
kuondolewa kwenye orodha ya wagombea kwenye uchaguzi unaotarajiwa
kufanyika hivi karibuni.Wanachama hao ambao walizubguka jengo hilo na
kutaka wapewe sababu za msingi kwanini wambura ameondolewa huku wakitaka
kufanya vurugu lakini vyombo vya usalama waliwahi kufika eneo la tukio
na kuweza kuwatuliza wanachama Hao.
No comments:
Post a Comment