Rais wa Nigeria Goodluck
Jonathana ameagiza shule zote na ofisi za serikali katika mji mkuu wa
Abuja nchini humo zifungwe wakati wa siku tatu za Mkutano wa Uchumi wa
Dunia World Economic Forum utakaanza nchini humo jumatano ijayo.
Serikali imesema hatua hiyo ni kuarahisisha
misafara ya magari. Lakini suala la kuimarisha ulinzi huenda ni mambo
yaliyosababisha hatua hiyo Mwandishi wa BBC Will Ross anasema akiwa
Abuja.Ulinzi mkali umehaidiwa kwa wageni wapatao 1000 wakati wa mkutano huo.
Rais Jonathan amesema polisi wapatao 5000 na wanajeshi watafanya doria na kushika hatamu za ulinzi wakati wa mkutano huo utakaoanza wiki ijayo.
Waziri Mkuu wa China Li Keqiang na Marais wa Rwanda, Senegal na Kenya ni miongoni mwa viongozi wa juu wa nchi watakaohudhuria.
Mji wa Abuja katika siku arobaini zilizopita ulishambuliwa kwa matukio mawili ya mabomu yaliyoua watu wapatao tisini na Boko Haram wanahusishwa na mashambulizi hayo.
Jina la kundi hilo lenye tafsiri ya "Kupiga marufuku elimu ya nchi za Maghiribi" kwa lugha ya Kihausa kimekuwa kikiendesha mashambulizi kadhaa kaskazini mwa Nigeria katika siku za hivi karibuni.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry ambaye anafanya ziara barani Afrika amesema Marekani itafanya kila liwezekanalo kuisaidia serikali ya Nigeria kuwaokoa na kurudisha nyumbani wasichana mia mbili waliotekwa na kundi la waislamu linalosadikiwa kuwa la Boko Haram siku kumi tisa zilizopita.
No comments:
Post a Comment