Pages

Friday, June 27, 2014

DADA ALIEKUWA AKIMNG'ATA BINTI WA KAZI AENDELEA KUSOTA RUMANDE

 
Anaitwa Amina Maige au Amina kumeza
Mkazi wa Mwananyamala, Amina Maige (42) jana alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni kujibu shtaka la kumjeruhi kwa meno mfanyakazi wake wa ndani Yusta Lucas.Amina akiwa amevalia vazi la baibui na kujifunika usoni kwa nikabu hali iliyosababisha kutoonekana sura kabla ya kuamriwa na Mwendesha Mashtaka ajifunue, alifikishwa mbele ya Hakimu Yohana Yengola ambapo alikana shitaka linalomkabili.
Yusta dada wa kazi alokuwa akiteswa na boss wake kwa muda wa miaka mitatu. Boss mwenyewe ndio huyo bidada hapo juu wala hafananii na unyama alokuwa akiufanya kwa mtoto wa watu.
Wakili wa Serikali, Tumaini Mfikwa akisoma hati ya mashtaka alidai katika kipindi cha kati ya 2012  na 2014 katika eneo la Mwananyamala kwa Manjunju, Amina huku akijua kufanya hivyo ni kinyume na sheria, alimjeruhi Yusta kwa kumng’ata sehemu mbalimbali za mwili na kumsababishia majereha makubwa.
Yupo segerea hivi sasa na na jana kesi yake ilisomwa.
Mfikwa alidai upelelezi umekamilka na aliomba tarehe ya kusikilizwa pamoja na mahakama kutotoa dhamana kwa mtuhumiwa kwa kuwa hali ya usalama wake ni tete.
Hakimu Yongolo alikubaliana na ombi hilo na mtuhumiwa alirudishwa rumande  hadi Julai 10, mwaka huu, kesi yake itakapoanza kusikilizwa.
Amina ambaye ni mtaalamu wa kompyuta katika kampuni ya Ocean Air Flight, aliiomba mahakama impe dhamana  akapate matibabu kwa kuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo, wakili Mfikwa aliiambia Mahakama kuwa mtuhumiwa atapatiwa matibabu akiwa rumande.
Juni 12, mwaka huu  wakati Amina anafikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza, shughuli katika mahakama hiyo zilisimama kwa takribani saa mbili baada ya watu waliokusanyika ndani na nje kutaka kumuona na kuanza kuzomea na kupiga kelele za kumtaka ajifunue uso.

No comments:

Post a Comment