Pages

Thursday, June 26, 2014

ZITTO KABWE ASEMA YAKE YA MOYONI BAADA YA ALBERT MSANDO KUZUSHIWA KUWA SIO MTANZANIA

Albert Msando na Zitto Z. Kabwe
LEO Albert Msando Alberto ALIPOST KUPITIA FACEBOOK JUU YA KUHOJIWA KWA BABA YAKE NA KAKA YAKE KUHUSU URAIA WAKE.NAYE ZITTO ALITOA YEKE YA MOYONI.TUANZE NA MANENO YA Albert Msando Alberto KISHA YATAFUTA YA ZITTO.
Leo tarehe 26.06.2014 nimepeleka maelezo yangu ofisi ya Uhamiaji Moshi kuhusu uraia wangu. Kwa maelezo niliyopewa awali kuna wanaosema mimi sio Mtanzania.
Kufuatia hiyo Mzee wangu, Gaspar Mwaria Msando na kaka yangu George Mwaria Msando wamehojiwa leo kama wananifahamu.
Miaka 34 baada ya kuzaliwa hospitali ya serikali, kusomeshwa shule msingi ya serikali, shule ya sekondari ya serikali na chuo kikuu cha serikali leo natakiwa kuelezea kama ni raia.
Najiuliza, kama sio raia narudisha gharama zote za serikali? Je naenda wapi kama leo hii mimi sio raia? Stateless person?
‪#‎Wonders ‪#‎Amazing
 BAADA YA MANENO HAYA YA ALBERT MSANDO ZITTO ALIANDIKA HAYA:

Eti Albert Msando Alberto sio raia wa Tanzania! Hii nchi ni vichekesho. Albert wanajua wanayemtafuta. Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Bwana Maswi aliwaambia Jukwaa la Wahariri kuwa Mimi Zitto Z Kabwe ni mkongo. Albert, watakusumbua sana. Tutawashinda tu. Hatushindwi vita

No comments:

Post a Comment