Pages

Friday, June 27, 2014

MAKAMU WA RAIS WA CHINA AMALIZA ZIARA YAKE NCHINI NA KUREJEA NCHINI KWAO


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao (kushoto) pamoja na Makamu wa Rais wa Tanzania, Mhe, Dkt. Gharib Bilal (kulia) wakipeana maneno ya mwisho katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam ikiwa ishara ya kuagana baada ya kumaliza ziara yake ya siku sita.



 Kikundi cha ngoma kikicheza mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao (hayupo pichani) wakati wa kumuaga baada ya kukamilisha ziara yake ya siku sita nchini Tanzania.



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao akimpa mkono wa shukurani Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara kabla ya kuanza safari yake ya kurudi nchini kwake.



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao akiwa amekumbatiana na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa Tanzania, Mhe, Dkt. Gharib Bilal ikiwa ishara ya kuagana mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku sita nchini Tanzania.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao akiondoka kuelekea kupanda ndege ya Qatar Airways kwa ajili ya kurudi kwao China. PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.

No comments:

Post a Comment