Pages

Monday, June 2, 2014

HALI ILIVYO BAADA KITUO CHA DALA DALA CHA MWENGE KUHAMISHIWA MAKUMBUSHO JIJINI DAR ES SALAAM


 Abiria wakiwa wanashangaa Daladala zinapita Mwenge Bila kusimama. Mabasi ya abiria yamezuiliwa kuendelea kuingia Kituo cha Mwenge ili kupisha zoezi la ubomoaji wa kituo hicho na badala yake sasa magari yanatakiwa kupakia na kushusha abiria Kituo cha Makumbusho.


 Daladala zikiwa zinapita bila kusimama wala kupakia sehemu yoyote.


 Kituo cha kwenda Tegeta , Kawe na Mbezi kikiwa Kitupu.


 Kituo cha Mabasi cha Mwenge Cheupe hakuna Daladala hata moja.


 Bajaji ndizo zimegeuka kuwa daladala ambapo sasa kila abiria alitozwa kiasi cha Sh. 1000 hadi Mwenge.


 Eneo la Kituo likiwa wazi bila daladala.


Ni heka heka za Bajaji kupiga kazi.....


 Bajaji zikiendelea na Kazi


 Upande wa Mwenge kwenda Morocco Pia hakuna mabasi hayasimami


 Hali ya utulivu Mwenge


 Eneo la Kituo cha Mwenye likiwa wazi bila magari kama ilivyozoeleka.


 Abiria wakingoja usafiri uliokuwa wa taabu nyakati hizo za asubuhi.


 Wafanya Biashara Wadogo wadogo wakianza kujikusanya kwa ajili ya kujadili jinsi ya kuanza Mgomo na kushinikiza kugomea ushuri.


 Wafanya biashara wakiwa wanaendelea kukusanyika ili kuandaa Mgomo wao.


 Kulia ni Meza moja ya Biashara ikibebwa ili kuwekwa katikati ya Kituo kama ishara ya kuanza mgomo rasmi na kushinikiza kuwa waanze Biashara zao hapo kama kawaida na kutotaka ushuru wa kulipia pesa nyingi.

Mpaka tunaondoka eneo la tukio Polisi walishawasili kuanza Doria  na kulinda usalama.
 Kibao kikionyesha kuwa hakuna kituo chochote kutoka Mwenge hadi Lufungila. Lufingila ndio Kituo Cha Kwanza ukiwa unatokea Mwenge kuelekea Ubungo.
 Ndani ya Kituo Cha Mwenge hakuna Msongamano tena wa Magari

No comments:

Post a Comment