Pages

Sunday, June 1, 2014

TAIFA STARS YASONGA MBELE KUWANIA KOMBE LA MATAIFA HURU YA AFRIKA

Photo: Timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imefanikiwa kuvuka hatua ya kwanza ya michuano ya kuwania kucheza michuano ya kombe la mataifa huru ya Afrika linalotarajiwa kufanyika mwakani.

Stars leo ilikuwa inacheza Zimbwabwe kwenye mchezo wa marudiano baada ya kuwafunga Zimbwabwe 1- 0 uwanja wa taifa wiki moja iliyopita, kwenye mchezo huo Stars imefanikiwa kufuzu baada ya kulazimisha sare ya 2-2.

Zimbwabwe walianza kufunga dakika ya 24, kabla ya Stars kusawazisha dakika kadhaa baadae kupitia Nadir Haroub 'Cannavaro' dakika ya 28. 
Muda mchache baadae  Thomas Ulimwengu aliongezea Tanzania bao la pili dakika ya 46, kabla ya dakika 10 baadae Zimbwabwe kusawazisha na kufanya matokeo 2-2.

Mpaka refa anapuliza kipenga cha mwisho matokeo yalibaki 2-2, na sasa Tanzania wanaingia hatua ya pili ambapo watacheza na Msumbiji.

Timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imefanikiwa kuvuka hatua ya kwanza ya michuano ya kuwania kucheza michuano ya kombe la mataifa huru ya Afrika linalotarajiwa kufanyika mwakani.

 Wachezaji wa Taifa Stars wakijipa morali ya ushindi kabla ya kuanza kwa mtanange huo dhidi ya Zimbabwe.
 Sehemu ya mashabiki wa Taifa Stars walioambatana na timu na baadhi ya Watanzania waishio Harare, wakishangilia kuisapoti Taifa Stars.
 Kiungo wa Taifa Stars, Frank Domayo akimtoka beki wa Zimbabwe.

Stars leo ilikuwa inacheza Zimbwabwe kwenye mchezo wa marudiano baada ya kuwafunga Zimbwabwe 1- 0 uwanja wa taifa wiki moja iliyopita, kwenye mchezo huo Stars imefanikiwa kufuzu baada ya kulazimisha sare ya 2-2.

Zimbwabwe walianza kufunga dakika ya 24, kabla ya Stars kusawazisha dakika kadhaa baadae kupitia Nadir Haroub 'Cannavaro' dakika ya 28. 
Muda mchache baadae Thomas Ulimwengu aliongezea Tanzania bao la pili dakika ya 46, kabla ya dakika 10 baadae Zimbwabwe kusawazisha na kufanya matokeo 2-2.
Mpaka refa anapuliza kipenga cha mwisho matokeo yalibaki 2-2, na sasa Tanzania wanaingia hatua ya pili ambapo watacheza na Msumbiji.

No comments:

Post a Comment