Uwanja wa JAMHURI mkoani
Morogoro utatumika kumuaga mtoto Nasra Mvungi aliyefariki jana alfajiri hospitali ya
Muhimbili.
Hayo yamesemwa na Ofisa
ustawi wa jamii mkoani Morogoro, Oswin Ngungamtitu.
Amesema idara hiyo kwa
kushirikiana na jeshi la Polisi imepanga kusimamia mazishi ya mtoto
Nasra Mvungi (4) maarufu katika magazeti kama mtoto wa boksi.
Mtoto huyo alifariki
dunia Jana katika hospitali ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kutokana na magonjwa
mbalimbali yanayosadikiwa kusababishwa kwake ndani ya boksi kwa zaidi ya miaka
mitatu.
Aidha kaimu kamanda wa
polisi mkoa wa Morogoro John Laswai alisema kuwa baada ya kifo cha mtoto
huyo taratibu za kipolisi
zitafanywa ikiwa ni pamoja na kupata taarifa ya daktari ambayo itaeleza sababu
za kifo cha mtoto huyo.
Alisema kuwa taarifa hiyo
ikishatolewa itapelekwa kwa wanasheria ambaye ataipitia na kuangalia sheria
inavyosema na kama taarifa hiyo itaeleza sababu za kifo kuwa imetokana na
ukatili na watuhumiwa hao basi watakamatwa na kesi itabadilika.
No comments:
Post a Comment