Pages

Wednesday, June 25, 2014

HUU NDIO UKWELI KUHUSU TAARIFA ZA KIFO ZINAZOMUHUSU WAZIRI SHUKURU KAWAMBWA


kutokana na mitandao ya kijamii muda mchache uliopita kuandika habari juu ya kumuhusisha na kifo mbunge Shukuru kawambwa mtandao huu umezungumza na watu wa karibu wa waziri huyo na kudai kuwa shukuru kawambwa ni mzima wa afya na habari zinazoenea ni uzushi mkubwa na hazina ukweli wowote.

           Na hii ndio messege kutoka Kwa mbunge RIDHIWAN KIKWETE juu ya uvumi huo.


    Ndg Watanzania,WanaBagamoyo na wapenda maendeleo, kwa niaba ya CCM-Bagamoyo na Ofisi ya Mbunge-Jimbo la Bagamoyo napenda kuleta kwenu Masikitiko yetu kwa niaba ya Chama na Familia ya Mheshimiwa Mbunge Shukuru Jumanne Kawambwa kutokana na Usumbufu ambao umesababishwa na habari zinazoenezwa Mitandaoni kwamba Mheshimiwa Kawambwa amekumbwa na Umauti akiwa njiani anaelekea Mwanza.


                UKWELI

        Mheshimiwa Shukuru Jumanne Kawambwa yupo Nchini Canada Akitimiza majukumu yake. Hivyo Watanzania na wana Bagamoyo mnaombwa radhi kwa usumbufu uliotokea na kwamba Mheshimiwa Mbunge yuko na Afya njema na utekelezaji wa Majukumu unaendelea kama kawaida.
Ndg.Ridhiwani Kikwete (Mnec)
Mbunge -Chalinze

No comments:

Post a Comment