Pages

Thursday, June 26, 2014

RAIS UHURU KENYATTA NI KINARA KWENYE MTANDAO WA TWITTER BARANI AFRIKA

Rais Kenyatta amempiku Paul Kagame wa Rwanda kwa idadi ya wafuasi kwenye Twitter.
Rais wa Kenya uhuru Kenyatta ndiye Rais anayejishughulisha zaidi kwenye mtandao wa Twitter barani Afrika.
Kenyatta amempiku Rais wa Rwanda Paul Kagame na mwenzake wa Afrika Kusini Jacob Zuma.
Kenyatta ambaye amekuwa mamlakani tu kwa mwaka mmoja, amejipatia wafuasi 456,209, yuko mbele ya mwenzake wa Rwanda Paul Kagame mwenye wafuasi 408,353 ambaye amekuwa mamlakani tangu mwaka 2000, miaka sita kabla hata ya Twitter kuanzishwa.
Rais wa Afrika Kusini anayesifika kwa kashfa mbali mbali, Jacob Zuma ana wafuasi 325,896 akishikilia nafasi ya tatu.

No comments:

Post a Comment