familia
ya denti wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, marehemu Sekabenga Pius
Mwakimenya (21) kilichotokea hivi karibuni na kugubikwa na utata,
imeanika ukweli kuhusiana na tukio hilo.Akizungumza na Uwazi, mwishoni
mwa wiki iliyopita katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, baba mdogo wa
marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Joseph Mwigune alisema, taarifa
waliyopewa na daktari aliyemfanyia uchunguzi inamaliza utata na
minong’ono yote inayoendelea chuoni.
Alisema,
kwa mujibu wa ripoti hiyo, kifo cha Sekabenga kimetokana na mzunguko wa
damu katika mishipa kutokuwa sawa, jambo lililosababisha ajisikie
vibaya na hatimaye kufariki dunia.
“Daktari
amesema kwamba mishipa ya damu haikuwa ikifanya kazi vizuri hali
iliyomsababishia ajisikie kuchoka kwa sababu damu haikuwa ikifika sehemu
zote za mwili wa marehemu,” alisema Mwigune.
Uwazi
lilifunga safari hadi chuoni na kuzungumza na baadhi ya wanafunzi ambao
walionyesha wasiwasi kuwa huenda marehemu aliamua kujiua kwa sumu kwa
maelezo kuwa, siku chache kabla ya kifo chake alionekana mwenye mawazo
mengi.
“Hakuwa
mwenye furaha, ni kama alikuwa na jambo zito linalomsumbua ndiyo maana
unasikia wanafunzi wengi hapa chuoni wanahusisha kifo chake na sumu,”
alisema denti mmoja kwa sharti la kutotajwa jina lake.
Hata
hivyo, taarifa kutoka kwa familia inayonukuu ripoti ya daktari inaziba
minong’ono yote kwa kuwa haionyeshi mahali popote kuwa marehemu alijiua
kwa sumu.
Marehemu
Sekabenga alikuwa mwaka wa pili chuoni hapo akichukua Shahada ya
Kwanza ya Biashara na Uhasibu, mwili wake umesafirishwa Jumamosi Mei
31, mwaka huu kwenda mkoani Mbeya kwa maziko yaliyotarajiwa kufanyika
jana Jumatatu.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Amina
Chanzo: Global Publisher.
No comments:
Post a Comment