Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania akizungumza na waandishi wa
habari wakati akitangaza kujiuzuru kwa Sitti Mtemvu aliyekua Miss
Tanzania 2014 baada ya kuzuka Sintofahamu kuhusu Umri wake, Lundenga
amesema Sitti Mtemvu aliandika barua ya kujivua taji na kuiwasilisha kwa
kamati ya Miss Tanzania Novemba 5 2014 ambapo kamati hiyo imeridhia
kujiuzulu kwake na kumvua taji.Hivyo taji hili na majukumu ya Miss
Tanzania sasa yatachukuliwa na mshindi wa pili Lilian Kamazima aliyekaa
kushoto katika picha ambaye taratibu za Miss Tanzania zinamruhusu
kuchukua jukumu hilo, Hashim Lundenga ametangaza uamuzi huo wakati
akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya JB Belmonte jijini
Dar es salaam leo.
Miss
Tanzania 2014 Lilian Kamazima akizungumza na waandishi wa habari
kuelezea furaha yake baada ya kamati ya Miss Tanzania kumvisha taji hilo
kutokana na kujiuzuru kwa Sitti Mtemvu aliyekuwa Miss Tanzania, Kulia
ni Hashim Lundega Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania.Hashim
Lundega Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania akionyesha barua
iliyowasilishwa kwa kamati hiyo na Bi. Sitti Mtemvu mara baada ya
kujiuzulu Umiss Tanzania na kujivua taji hilo.
No comments:
Post a Comment