Katibu Mtendaji Bodi
ya Filamu Bibi Joyce Fisoo akizungumza na wasanii wa bongo movie wanaotarajia
kwenda nchini Uingereza kurekodi filamu na kampuni ya Didas Entertainment
iliyopo nchini Uingereza. Kulia ni Mama wa Didas Bi. Nuru Idrisa
Kutoka kulia Msanii
Yusuph Mllela, Afisa kutoka Bodi ya Filamu Bibi Beatrice Msumari, Msanii Esha
Buhet na Msanii Husna Athumani wakimsikiliza kwa makini Katibu Mtendaji Bodi ya
Filamu walipofika ofisini kwake kwa ajili ya kuwaaga wasanii hao wanaotarajia kwenda
nchini Uingereza kurekodi filamu na kampuni ya Didas Entertainment.
Katibu Mtendaji Bodi
ya Filamu Bibi Joyce Fisoo kulia akimpa mkono msanii Yusuph Mllela baada ya
neno la kuwaaga wasanii watatu (Yusuph Mllela, Esha Buhet na Husna Athumani) wanaotarajia
kwenda nchini Uingereza kurekodi filamu na kampuni ya Didas Entertainment.
Msanii wa Bongo Movie Bi. Esha Buhet kushoto
akifurahi wakati wa kuagana na Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi Joyce Fisoo
kwa ajili ya kuanza safari ya kwenda nchini Uingereza kurekodi filamu na
kampuni ya Didas Entertainment. Katikati ni Mama wa Didas Bi. Nuru Idrisa.
Msanii Husna Athumani akipokea mkono wa pongezi kutoka kwa Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi Joyce Fisoo (kulia) wakati wa kuwaaga wasania wanaotarajia kwenda nchini Uingereza kurekodi filamu na Kampuni ya Didas Entertainment. Katikati ni Mama wa Didas Bi. Nuru Idrisa. (Picha zote na: Genofeva Matemu – Maelezo)
No comments:
Post a Comment