Mchungaji
Kiongozi wa Kanisa la Uzima na Ufufuo, Josephat Gwajima amejisalimisha
kituo cha polisi kati kuhojiwa juu ya kutoa lugha chafu dhidi ya Askofu
Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp
Kardinali Pengo.
Mchungaji Gwajima anadaiwa kumkadhifu na kumtukana hadharani Kardinali Pengo.
Inadaiwa
matusi hayo yameonekana kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ya
WhatsApp na mingineyo, ambapo kuna sauti iliyorekodiwa na picha za video
zikimuonyesha Mchungaji Gwajima akimkashifu na kumtukana kwa maneno
makali Kardinali Pengo katika hali ambayo pia imewaudhi watu wengine.
No comments:
Post a Comment