Pages

Monday, November 3, 2014

MAKONDA AKANA KUMPIGA JAJI WARIOBA


Katibu wa Uhamasishaji Umoja wa Vijana wa CCM, Paul Makonda akionesha kwenye simu yake picha ya video iliyopigwa wakati wa vurugu zilizotokea wakati wa mdahalo wa kujadili raismu ya Katiba inayopendekezwa, kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza  jana, ambapo Makonda aliyedaiwa kump[iga aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Waziri Mkuu wa zamani Jaji mstaafu Joseph Warioba, amekanusha kumpiga leo katika mkutano wa waandishi wa habari, Dar es Salaam. Pia Makonda amesema kuwa ahwezi kabisa kudiriki kumpiga kwani anamheshimu kama babake mzazi. Amesema kuwa hata leo asubuhi amezungumza na warioba kwenye simu kumjulia hali. Warioba naye amekanusha kupigwa na Makonda wala mtu yoyote kwenye vurugu hizo.
Makonda akisisitiza jambo katika mkutano huo ambapo pia aliwaambia kazi kubwa aliyoifanya wakati wa vurugu hizo, ni kumsaidia Warioba kutoka salama pamoja na Mwanasiasa mwenye ulemavu wa macho ambaye pia alikuwa anamuokoa ili asipatwe na dhahama hiyo.

Makonda akiendelea kuelezea kuwa anasikitishwa na vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii iliyomzulia kwamba yeye ndieye aliyesababisha vurugu wakati siyo. Pia amelaani watu wote waliosababisha vurugu hizo kwamba kitendo hicho kinadhoofisha demokrasia nchini.

No comments:

Post a Comment